ILIPOISHIA
Kwanza
kijana huyo akamkumbatia raisi Praygod Makuya, nakumfanya raisi Praygod
Makuya kujitahidi kuvuta kumbukumbu zake niwapi alipo muona kijana huyu
anaye mwagikwa na machozi. Kumbukumbu za raisi Praygod Makuya zikagota
kwenye ndege na kukumbuka kijana huyu ndio yule aliye kuwa akishirikiana
na Rahab.
“We…weee si…”
Raisi
Praygod alizungumza kwa kigugumizi, kwani kama kijana huyu alimkosa
kwenye ndege basi leo amekuja kumuua kwenye alaiki ya watanzania.
“Samson, Samson muheshimiwa.”
Samson alizungumza huku machozi ya uchungu yakimwagika, akazidi kumkumbatia Raisi Praygod Makuya kwa nguvu zake zote.
ENDELEA
Raisi Praygod Makuya akajaribu kujitoa mikoni mwa Samson ila akajikuta akishindwa kwani Samson alizidi kumkumbata kwa nguvu
“Naoamba unisamehe muheshimiwaa”
Samson
alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi. Makamu wa rais
baada ya kumuona Samson, ikanyanyuka kwenye kiti chake huku macho
yakiwa yamemtoka. Woga wa siri yake kuweza kufichuliwa na mjomba wake
huyo ukaanza kumtawala.
“Muheshimiwa natambua kwamba nilikukosea, ila si kosa langu mimi”
“Nilitumwa
niweze kukuangamiza, na mjomba wangu ili kiti chako cha uraisi kiweze
kukaliwa na mjomba wangu ambaye ni makamu wa raisi wa sasa”
Maneno
ya Samson yakamfanya raisi Praygod kuweza kumtazama makumu wa raisi
aliye keti kwenye jukwaa. Sura ya makamu huyo ikamuashiria raisi
Praygod kwamba ina hasira dhidi yake.
“Nimekuelewa kijana, unaitwa nani?”
“Samson”
“Sawa Samson nitalifanyia kazi”
“Kabla ya hayo kuna jengine muheshimiwa nahitaji kukuambia”
Makamu
wa raisi alipo zidi kumuona Samson anazungumza na Raisi Praygod,
akazidi kushikwa na hasira akiamini kwamba kila kitu kimesha haribika,
akaangaza macho yake huku na huku, akamuona mlinzi wake aliye simama
pembeni, bastola ikiwa imechomekwa kiunoni. Kwa haraka makamu wa Raisi
akaichomoa bastola hiyo bila hata yakufikiria mara mbili, akafyatua
risasi ambazo kwa haraka Samson aliweza kuliona tukio hilo, alicho
kifanya ni kumsukumia pembeni Raisi Praygod, na risasi hizo mbili
zikaingia mwilini mwake na kumuangusha chini.
Mlio
wa bastola hiyo, ukazua hali ya taharuki kwa kila aliye kuwa katika
uwanja wa taifa, kila mmoja akafanya jinsi akili yake ilivyo muagiza
kuweza kufanya, wapo walio weza kuchanganya miguu yao na kukimbia hovyo
hovyo, wengine waliweza kupoteza fahamu, wengine waliweza kukanyagwa
vibaya pale walipo zidiwa nguvu na wale walio hitaji kuokoa nafsi zao.
Askari na walinzi wa viongozi waalikwa wakawa na kazi moja tu,
yakuwaokoa viaongozi wao waliomo ndani ya kiwana hichi kikubwa cha
mpira. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani hapakuwa na aliye weza kuvumilia.
Walinzi wengi wakamzunguka Raisi Praygod, wakamtoa uwanjani huku wakiwa
wanamkimbiza, baadhi ya wanajeshi wakaweza kumtia nguvuni makamu wa
raisi aliye weza kufanya tukio lakinyama.
Hali
ya Samson, ikazidi kuwa mbaya huku macho yake akimtizama jinsi Raisi
Praygod anavyokimbizwa na askari kuyaokoa maisha yake, Samson akaachia
tabasamu pana, huku taratibu macho yake yakiingiwa na ukungu ulio
pelekea kuyafumba macho yake na kutulia tuli.
***
Moja kwa moja Agnes akakimbilai kwenye chumba amacho aliamini kiongozi
anaye muhitaji ni lazima atakuwa amepelekwa huko baada ya milipuko hiyo
ya magari kuweza kutokea. Akafanikiwa kufika kwenye kordo yakuelekea
kwenye chumba hicho kilichopo chini ya ardhi. Walinzi walio valia suti
nyeusi pamoja na miwani nyeusi wapatao kumi na tano, wakawa wamesimama
nje ya mlango huo huku macho yao yote wakimtupia Agnes anayekuja kwa
kasi huku akiwa amejiamini sana.
Kila
mmoja akabaki kuwa na alama ya kujiuliza kwani mavazi aliyo yavaa Anges
ni ngumu sana kumtilia mashaka kwani akafanana sana na wahudumu wa
kikosi cha kuzima moto. Muonekano wa umbo dogo dogo la Agnes, likawapa
imani kwamba binti huyo anaye kuja kasi huku akiwa amenyanyau mikono
yake juu, hana madhara yoyote kwao.
“Naomba muwatoe viongozi nje, jengo limeanza shika moto”
Kauli
ya Agnes aliyo izungumza kwa lugha ya kirasia, ikawafanya walinzi wote
kuchanganyikiwa, ikawalazimu kuwasiliana na wezao waliomo ndani ya
chumba kuweza kuwatoa viongozi hao haraka iwezekanavyo. Bwana Paul Henry
Jr pamoja na Raisi wa Russia wakatolewa ndani ya chumba hicho kuku
wakiwa wamezungukwa na walinzi wao wapatao ishirini.
“GO GO GO….!!!”
Mlinzi
mmoja alizungumza huku akionekana ndio mkuu wa kikosi hichi maalumu
chakuwalinda viongozi hawa. Agnes akatazama jinsi walinzi hawa walivyo
makini na kuwalinda viongozi hawa.
“Hapa hapa”
Agnes
akawaacha viongozi hao kupiga hatua nyingi mbele, kisha kwa kasi
akanza kukimbia na kuwafwata kwa nyuma, akamfikia mmoja aliye ishika
bastola yake na kuitanguliza mbele. Kwa kasi ya ajabu Agnes akajigeuza
kwenye shingo ya mlinzi huyo na kuivunja, kabla hajaanguka chini, tayari
akawa ameikamata bastola ya mlinzi huyo.
Kwa
mafunzo ya uharaka na umahiri wake katika kutumia silaha hizi za
bunduki, Agnes, akaanza kuwaangusha chini walinzi hao, walio
changanyikiwa kwani, kitendo cha mtu kujaribu kufanya shambuliza tayari
umesha vamiwa na kuangushwa chini.
Agnes
akafanikiwa kusimama nyuma kwa bwana Paul Henry Jr, akampiga kabali
huku bastola yake akiwa ameiweka sikioni mwa kiongozi huyo. Macho yake
kwa haraka aliweza kuona miili ya walinzi wapatao kumi na sita wakiwa
chini wamekufa huku wanne wakiwa wamesimama huku wamenyooshea bastola
zao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment