Katika kile kinachoonekana viongozi wa serikali kuvutiwa na jinsi
Diamond na lebel yake WCB wanavyoibadilisha tasnia ya muziki wa Tanzania
kuwa fursa ya kibiashara na kazi rasmi, Mh. Waziri wa wizara mambo ya
ndani, Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea ofisi za WCB na kukutana na
baadhi ya wafanyakazi na wasanii wa label hiyo ili kuwapa moyo na
kuwahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakisha kazi zao
zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Pia kawaambia kuwa serikali haitasita
kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.
Binafsi nimeona ni jambo jema hasa ukizingitia wameshatembelea viongozi na mawaziri kadhaa. Rai yangu kwa wasanii wengine kuiga mfano wa WCB katika kuwa na ofisi maalumu na kuzipa thamani kazi zao.
Binafsi nimeona ni jambo jema hasa ukizingitia wameshatembelea viongozi na mawaziri kadhaa. Rai yangu kwa wasanii wengine kuiga mfano wa WCB katika kuwa na ofisi maalumu na kuzipa thamani kazi zao.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment