Loading...

MWIMBAJI Rich Mavoko Achekelea Wimbo Wake Kuchezwa Radio za Uingereza


Kokoro umekuwa wimbo wa kwanza katika career ya Rich Mavoko kuchezwa na vituo vya redio vya nchini Uingereza vikiwemo #BBCRadio #1Xtra na #CapitalXtra.

@Richmavoko ameiambia amesema kuwa hayo ni mafanikio makubwa kwake.
.
“Katika ndoto zangu nilikuwa nafikiria nije kufanya kitu ambacho kitatoka nje ya mipaka, kufika west, kufika south, kufika sehemu ambazo nawaona wasanii ambao nawatamani wanafanya kazi kubwa wanafika,” amesema.

Mavoko amesema Kokoro ambao amemshirikisha @diamondplatnumz, ni wimbo wenye ladha ambazo hajawahi kufanya lakini risk aliyoifanya imezaa matunda.
.
“Namshukuru Mungu nimeona matunda yake, BBC sijawahi kuchezwa haki ya Mungu. Nimetumiwa nikiwa huku Marekani nikasema noma noma,” ameongeza Mavoko kwa furaha kubwa.

Muimbaji huyo amesisitiza kuwa kwa sasa ana hasira kubwa zaidi ya kuhakikisha anafika katika masoko ambayo hakuwahi kufika kwa kuachia kazi kali zaidi.
.
“Nataka niingie kwa nguvu,” anasema. “Nataka niingie nikiwa nachop muziki wa aina tofauti tofauti. Bado nitastick kwenye Bongo Flava kwasababu ndio muziki wa nyumbani, ndio maana #Kokoro home itafanya vizuri, nje itafanya vizuri kwasababu naweza nikafanya vitu vingi kwenye wimbo mmoja.”

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top