Ligi Kuu soka Ubelgiji iliendelea usiku wa December 21 2016 kwa michezo
kadhaa kuchezwa, timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana
Samatta ilikuwa mgeni wa timu ya Zulte-Waregem katika uwanja wa
Regenboog.
KRC Genk ikiwa ugenini imekubali kupoteza mchezo kwa goli 1-0, goli
ambalo lilifungwa na Souahilo Meite dakika ya 26 ya mchezo, kwa matokeo
hayo KRC Genk wanakuwa na takwimu kwa mechi zao 5 zilizopita kushinda
mechi 2, kufungwa mechi 2 na kutoka sare mchezo mmoja.
Kwa upande wa Mbwana Samatta kocha wake Peter Maes ameendelea kumuamini
na kumpanga kwa dakika zote 90, mchezo uliyopita Genk walilazimishwa
sare ya kufungana goli 2-2 na Standard de Liege goli la pili la
kusawazisha la Genk lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 78.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment