Uchaguzi wa kumpata Meya wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, umefanyika na hatimaye Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Maabadi Hoja amechaguliwa kuwa Meya wa kwanza.
Uchaguzi huo ulifanyika jana kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando, ambaye alikuwa msimamizi
wa uchaguzi, alisema mgombea huyo wa CCM ndiye aliyeshinda.
Washiriki
wengine walitoka vyama vya CCM, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Mhando alisema Hoja alipata kura tisa
dhidi ya Celestine Maufi (CUF) aliyepata kura tano na kura moja
iliharibika.
Pia,
Mhando alisema katika uchaguzi huo, Amini Sambo ambaye ni Diwani wa
Kata ya Kibada, pia kutoka CCM, alishinda nafasi ya Naibu Meya, akipata
kura 10 dhidi ya Ernest Mafimbo wa CUF, aliyepata kura tano.
“Tunashukuru uchaguzi umefanyika vizuri Kigamboni, sasa tumepata Meya na
Naibu Meya,” alisema Mhando.
Uchaguzi
wa Meya na Naibu wake kwa upande wa Kigamboni, umefanywa baada ya
Wilaya ya Temeke kugawanywa na kuwa wilaya mbili za Temeke na Kigamboni.
Mhando
alieleza kuwa uchaguzi huo ambao ni wa mara ya kwanza kwa halmashauri
hiyo, ulifanyika kwa amani bila kuwapo na malalamiko.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment