Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga imemuhukumu kifungo cha miaka 25 ama
kulipa faini ya Sh 3.7 bilioni mfanyabiashara, Charles Kijangwa baada
ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.
Hakimu Mkazi, Cresian Kisongo ametoa hukumu hiyo leo kwa Kijangwa ambaye
aliruka dhamana tangu mwaka 2010, takribani miaka sita sasa.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya
Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Lushoto
kufanikisha jitihada za kumtafuta kwa kumkamata na kumkabidhi
mahakamani hapo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Saraji Iboru alidai mahakamani kuwa
mshtakiwa Kijangwa alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu
mwaka 2010 ambapo aliruka dhamana katika kesi ya uhujumu uchumi namba 6
ya mwaka 2007 iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na wenzake Michael Msuya
na Nyaisa Makori.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment