Loading...

Kalapina Amlaumu Mama Chid Benz Kwa Kumdekeza na Kumwendekeza Chid Benz Mpaka Ameshindwa Kuacha Madawa


Rapa Kalapina ambaye ni mwanaharakati wa kuwasaidia watu ambao wameingia kwenye matumzi ya dawa za kulevya amefunguka na kusema kuwa mama yake mzazi Chid Benz kama mtu anayemuendekeza Chid na kumfanya asitoke kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Kalapina amesema mama huyo anampenda sana mtoto wake kiasi cha mtoto kujua na kuona kwamba hata akifanya jambo fulani yupo mama yake ambaye atasimama na yeye.

Kalapina alisema hayo jana kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wazazi wengi wamekuwa chanzo cha watoto wao kuingia kwenye matumzi ya dawa za kulevya na kuingia hata kwenye mahusiano ya jinsi moja sababu ya wazazi wamekuwa wakiwadekeza sana watoto au kuwapa uhuru mkubwa na kuruhusu maisha ya uzungu kutawala.

"Kiukweli mama yake mzazi Chid Benz anampenda sana mwanaye na hali hiyo inampelekea mdogo wangu yule kuona hata nikizingua mama atanitafuta tu, au kuona mama atasimama na yeye tu sababu mama yake anampenda sana, lakini siyo Chid Benz tu wazazi wengi wanawalea watoto kwa kuwadekeza sana, wazazi hawana muda na watoto na hili linachangia vijana kuingia kwenye madawa ya kulevya hata kwenye ushoga pia, lakini sisi wazazi wetu zamani ulikuwa ukizingua unapigwa sana hivyo lazima utanyooka tu" alisema Kalapina.

Source:EATV

Wakurugenzi TANESCO Wasimamishwa Kazi, Mmoja Ajiuzulu!


Wakuu huku Tanesco hali si shwari mpaka sasa Wakurugenzi wetu watatu wameshushwa vyeo na kuhamishiwa katika chuo cha TANESCO (TSS).

Declan Mhaiki aliyekuwa Deputy Managing Director - Transmission
Sophia Mgonja aliyekuwa Deputy Managing Director - Distribution
Mr Kachwamba aliyekuwa Deputy Managing Director - Generation.

Aidha Watson Mwakyusa, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu yeye ameamua kuachia ngazi.

Source:Jamii Forums

Panga Lapita Tanesco...Habari Zilizopo Katika Magaeti Ya Leo Alhamisi ya January 5




Panga Lapita Tanesco...Habari Zilizopo Katika Magaeti Ya Leo Alhamisi ya January 5

Jeshi la Polisi Laua Majambazi Watatu Dar es Salaam


Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado hayajafahamika.

Alisema marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni 26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Hata hivyo, alipoulizwa ufafanuzi zaidi wa tukio hilo na je watuhumiwa hao walikuwa na usafiri gani, Sirro alisema kuwa hizo ni taarifa za awali na taarifa rasmi atazitoa leo.

Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa zaidi zinadai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha, ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.

Lakini, Polisi haijathibitisha taarifa hizo na imeeleza kuwa itatoa taarifa  zaidi leo.

Hali si Shwari Wolper na Harmonize....Meseji Aliyopost Wolper Yaonyesha Wameachana



Jacline Wolper ame post hii halaf ghafla kafuta, hii maana yake nini wadau?
Jisomee alichoandika kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Jike Shupa Awaanika Mastaa Anaowauza Kwa Vigogo, Yumo Wolper, Masogange



DAR ES SALAAM: Imefichuka! Wakati mastaa mbalimbali wakijinasibu mara kwa mara kupitia vyombo vya habari kuwa hawafanyi biashara ya kuuza miili yao kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amekiri kuwauza wenzake kibao kwa vigogo, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukujulisha.

Jike Shupa ambaye ni ‘video queen’ kwenye nyimbo mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, bila kujijua, amejikuta akiingia kwenye mtego wa kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers na kutaja idadi ya mastaa huku akieleza kila msanii ana dau lake tofauti, hakuna bei maalum.

ILIKUWA HIVI

Baada ya OFM kupata habari kutoka kwa vyanzo vyake mbalimbali kwamba mwanamama huyo anawauza wenzake, wakiwemo mastaa na kudaiwa kuwa ni kinara mkubwa wa biashara hiyo, OFM iliingia mzigoni na kupata majibu chanya.



AANZA KUINGIZWA KINGI

Makachero wa OFM waliwasiliana na Jike Shupa na mmoja wao akamuomba waonane ili aweze kupata huduma ya kuunganishwa na msanii atakayepatiana kwa bei ya wastani.

Jike Shupa baada ya kuelezwa hivyo alimuomba kachero huyo aliyejitambulisha kwake kama mfanyabiashara kuwa wakutane maeneo ya Kinondoni kwenye mgahawa mmoja maarufu majira ya saa moja usiku ili waweze kuzungumza vizuri kuhusu dili hilo.

OFM YAWAHI KUFIKA MGAHAWANI

Saa moja usiku kachero wa OFM alikuwa katika eneo la tukio, alipofika kwenye mgahawa huo alikaa na kumsubiri Jike Shupa ambaye aliingia na vijana wawili aliowatambulisha kuwa ni wadogo zake, ikiwa ni dakika 15 zaidi ya muda wa makubaliano.

OFM: Karibu sana Jike Shupa.

Jike Shupa: Asante, umenisubiri sana eeeh?

OFM: Yeah, lakini siyo tatizo.

Jike Shupa: Pole sana.


Baada ya Jike Shupa kukaa na mhudumu kumsikiliza anachohitaji (OFM ililipia bili yote), mazungumzo kati yake na OFM yalipamba moto na baada ya muda, alielezwa moja kwa moja kuwa dili alilotaka kumpa lilikuwa ni kumpata Amber Lulu ili awe naye kimapenzi, jambo ambalo lilionekana kuwa jepesi mno kwa Jike Shupa.

ATANGAZA DAU

Jike Shupa alimhoji OFM kama alikuwa na fedha za kutosha maana kazi yake yeye ‘anadili’ na watu wenye fedha tu na kwa kumuuza Amber Lulu, alisema atachukua shilingi milioni moja na nusu ikiwa ni nje ya fedha ambazo Amber Lulu atataka kulipwa.

‘MFANYABIASHARA’ FEDHA SI TATIZO

Kuonesha kwamba fedha si chochote, kachero wa OFM hakubisha juu ya hilo, alichofanya ni kumwambia kuwa nusu ya fedha alizokuwa anahitaji  angemlipa muda mchache wakati wakiendelea na mazungumzo, lakini akataka kujua kutoka kwa mwanamke huyo kama amewahi kuwauza mastaa wengine kama anavyofanya kwa Amber Lulu?


Jike Shupa: Wako wengi tu, ambao huwa ‘ninawa-connect’ (kuwaunganisha) na mabwana, mfano, (akataja jina la msanii mkubwa ambaye tunahifadhi jina lake kwa sababu hatukumpata), Tunda, Masogange, Wolper na wengine wengi.

ETI HAKUNA ANAYEMCHOMOLEA

“Hakuna staa wa kike ambaye simfikii, ni wewe tu kusema unamtaka yupi, unatoa pesa halafu mimi namaliza mchezo wote.

“Unawaona hata hao vijana niliokuja nao (anawanyooshea kidole walipokuwa wamekaa)? Hao ni mashoga, huwa nawaunganishia watu (wanaume) wanaowataka kufanya nao mapenzi.”


OFM YAMMWAGA KIAINA

Baada ya OFM kukamilisha upelelezi wake na kujiridhisha kuwa kweli Jike Shupa ni kuwadi na anawauza wasanii wenzake wa kike pamoja na mashoga kwa mapedeshee, ilimtoka ‘kisanii’ mwanadada huyo huku ikiwa na ushahidi wa kutosha.

WATUHUMIWA WAFUNGUKA

Alipotafutwa Masogange na kusomewa mashitaka yake, awali alianza kwa kusema hana urafiki kivile na Jike Shupa na kwamba waliwahi kukutana naye mara moja tu.


“Sina urafiki kivile, nachukia sana mtu kuzungumza kitu ambacho sijafanya, kwanza huyo Jike Shupa mwenyewe hana mtu wa kuniunganisha naye. Hebu ngoja nimpigie sasa hivi nimpe vidonge vyake, sipendagi ujinga mimi,” alisema Masogange na baada ya kumpigia na kumkosa, alimuandikia meseji ndefu Jike Shupa ya kumsuta ambayo aliikopi na kuipiga picha kisha kumtumia mwandishi wetu.

Jike Shupa hakujibu ujumbe huo wa kichambo ambao ulionesha umefika kwenye simu yake.

AMBER LULU NAYE ANENA

Kwa upande wake Amber alikanusha vilivyo madai hayo ya kuuzwa na kama haitoshi, alisema hana hata urafiki naye.

“Huyo labda anatafuta kiki, sina hata urafiki naye ataniuza kivipi? Sinaga hizo habari,” alisema Amber.


WOLPER NAYE AMKANA

Alipotafutwa Wolper na kuelezwa kama amewahi kupigwa bei na Jike Shupa, alimkana kuwa hamtambui na kusema anaomba atumiwe picha ili japo amuone anafananaje, kwani watu wa aina hiyo anashindwa kuwaelewa awaweke kwenye kundi gani.

“Unajua kama ana akili timamu si mwezi mchanga, inabidi nidili naye na ikiwezekana nimshtaki maana atakuwa amenizushia jambo ambalo sijawahi kulifanya lakini kama ni mwezi mchanga (hajakamilika kiakili), naweza nikamsamehe,” alisema Wolper.

MASTAA ZAIDI WAFUNGUKA

Mastaa wa kike mbalimbali walipotafutwa na kuelezwa habari hizo kila mmoja alionesha kukasirika na kuzungumza lake.


BABY MADAHA

“Huyo Jike Shupa hawezi kuniuza mimi labda hao anaoonana nao na suala la kuuzwa ni la mtu binafsi huwezi kuuzwa kama ng’ombe.

“Huyo msanii ana uwezo wa kuwauza wale anaowamudu kwangu atagonga mwamba kwani hatuongei lugha moja, yaani viwanja ninavyoenda ni tofauti na vyake, wanaume anaokutana nao ni tofauti na wale nitakaokutana nao mimi, kwanza Kinondoni na Mbezi ni wapi na wapi?”

SHAMSA FORD

“Mimi nimeolewa hilo haliwezi kunitokea kabisa waulizeni hao ambao hawaeleweki nina mume ndani tayari.”

ISABELA MPANDA

“Huyo Jike Shupa hawezi kuniuza kwa sababu ninajitambua labda hao wengine na sina shida na siwezi kuuzwa kama karanga, huwa naenda kwa mwanaume ninayemtaka.”

ROSE NDAUKA

“Jamani hivyo ni vitu vya kipumbavu siwezi kuvizungumzia wala kumzungumzia mtu kama huyo.”

NENO LA MHARIRI

Kwa kuwa OFM imemnasa Jike Shupa ‘live’ akithibitisha madai ya kuwa anawauza wenzake, anapaswa kuachana na vitendo hivyo mara moja kwani vinakwenda kinyume na mila na desturi za Kitanzania.

Ni tabia ambazo zinakwenda kinyume na mafundisho ya imani za dini zote, ni wakati wa Jike Shupa na mastaa wenzake wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kikahaba kuachana navyo na kutafuta mkate wa kila siku kwa njia halali.

Stori: waandishi Wetu, Risasi Mchanganyiko, Jan 4-6, 2017, Toleo 1388

Madhara Ya Kuchaguliwa Mwenzi Wa Kuishi Naye Katika Mahusiano Ndoa


Ni imani yangu kuwa uko salama rafiki na unaendelea vizuri katika harakati zako za kila siku kuhakikisha unapata kile unachokitaka kwenye maisha yako. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo ameweza kutustahilisha tena kuiona siku hii ya leo. Kwa hiyo rafiki, tutumie muda huu wa leo vizuri kwani leo ni siku bora ambayo haitokuja tena kutokea katika maisha yetu hapa duniani.

Mpendwa rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja yale ambayo nimeweza kukuandalia siku hii ya leo. Hivyo basi, nakusihi ungana nami mwanzo hadi mwisho wa makala hii ili tuweze kusafiri wote kwa pamoja. Leo tutakwenda kujifunza juu ya madhara ya kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye kwenye maisha ya mahusiano. Je ni madhara gani rafiki? Karibu rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Katika moja ya matatizo yanayowasumbua watu duniani basi moja wapo ni mambo ya mahusiano. Mahusiano haya yanaweza kuwa mahusiano ya uchumba, mahusiano ya ndoa na nk. Sasa katika mahusiano ya ndoa wapo watu wengi sana wanaruka hatua muhimu sana ambazo baadaye zinakuja kuwaumiza vibaya. Hatua hizo muhimu ni urafiki na uchumba kwa hiyo, ikitokea watu wamekutana ndani ya miezi miwili, mmoja na kukimbilia kufunga ndoa ndio hawa wale wanaokuja kujuta kwa nini walifanya maamuzi hayo.

Mpendwa msomaji, malengo mahususi ya somo letu la leo ni madhara ya kuchaguliwa mwenza katika maisha ya mahusiano. Ziko jamii tofauti duniani zenye utaratibu au utamaduni wa kuwachanguliwa watoto wao wenza pale wanapokua wamekaribia ule umri wa kuishi ya maisha ya ndoa kama mke au mume. Wazazi wa jamii za kuwatafutia watoto wao wenza bado wapo mpaka leo katika zama hizi za taarifa na pengine unafahamu watu ambao wanafanya jambo hili kwenye jamii iliyokuzunguka.

Kwa mfano, mtoto tokea akiwa mdogo anawekewa ‘’ oda’’ mapema kuwa wewe utaolewa na mtu fulani au utamuoa mtu bila kujali unataka au la. Kwa hiyo, tabia hii inawanyima watoto wengi kuwa na mtu Yule anayempenda badala yake wanakuwa na watu ambao siyo chaguo lao la kutoka moyoni. Utamaduni huu unakuwa ni kama kumnyima mtu kuishi maisha anayotaka hapa duniani.
Unaporuhusu wazazi wakuchagulie mwenza wa kuishi naye katika maisha ya ndoa kwanza inakuwa ni utumwa wa hali ya juu. Kwanini?

Kwa sababu kuchaguliwa kufanya kitu ambacho hukipendi katika maisha yako ni utumwa. Vivyo hivyo, kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye ni utumwa pia. Unapokuwa unachaguliwa mwenza wa kuishi naye unakuwa unavunja hatua muhimu sana katika kuelekea maisha ya ndoa ambayo ni urafiki na uchumba. Kupitia hatua hizi unaweza kumchunguza mwenzako ni mtu wa namna gani, falsafa yake ya maisha ikoje, ni mtu chanya au hasi, ni mtu wa kuigiza maisha au ni mtu halisi anayeishi bila kuigiza maisha na mambo mengine mengi unayotaka kuyajua kutoka kwa mwenzako.

Rafiki, watu wanaoishi na wenza wao kwenye maisha ya ndoa kwa kuchanguliwa na kwenda kuanza kuishi maisha ya urafiki, uchumba na ndoa kwa wakati mmoja huwa wanashinda sana. unakuta mwenzako anaishi falsafa tofauti kabisa na wewe ulivyotarajia. kwa mfano, wewe falsafa yako ni kuishi chini ya kipato chako na unakuta mwenzako anataka kuishi juu ya kipato kwa kufanya mambo ambayo hayana ulazima kwenye maisha. Lakini kama ulikuwa umemgundua mwenzako na kumsoma vizuri katika hatua za uchumba ungeweza kufanya maamuzi mapema kwa kumpima kama mtu huyo anakufaa au la kulingana na vigezo vyako.

Kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye katika zama hizi ni aibu kwa kweli kwani ni kuchaguliwa kufanya chochote ambacho hukipendi ni utumwa katika maisha yako. Kumbuka rafiki, hata mzazi akikuchagulia mpenzi ambaye wewe humpendi na ukakubali utakua umejichagulia wewe mwenyewe kuingia shimoni. Kwa hiyo, hata wazazi wakikuchagulia kuishi na mwenza ambaye wanampenda wao ni kama kuchaguliwa maisha ya kuishi hapa duniani. Licha ya kuchaguliwa maisha wewe ndiye utakayeenda kuishi hayo maisha na wala siyo wazazi watakaopata raha au shida, ukiingia shimoni wao hawatakuwepo bali wewe ndio utawajibika.

Hatua ya kuchukua leo; usikubali kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye katika maisha yako. Ishi na mtu unayempenda kutoka moyoni, ishi na mtu ambaye mliweza kupitia hatua za urafiki, uchumba ukamjua vizuri tabia zake ni mtu wa namna gani. Fanya kitu ambacho unakipenda ndio furaha ya kweli katika maisha ambapo utapata mafanikio makubwa yenye furaha na ubora wa hali ya juu.

Kwa kuhitimisha, tunaishi karni ya ishirini na moja na hatuko tena katika zama za mawe bali tupo katika zama za taarifa. Kuwa chachu ya mabadiliko kwa kuvunja utumwa huo katika jamii uliyopo siyo unasoma na kupata elimu ya juu bado ukirudi nyumbani wazazi wanakushurutisha kuoa au kuolewa na mtu Fulani bila ya ridhaa yako mwenyewe. Wewe ndio mwenye maamuzi ya maisha yako kwa sababu hakuna mtu mwingine atakaye ishi maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe.
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top