Katika
muendelezo wa kuwapatia wateja wake na watanzania wote kwa ujumla
burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wasanii wa WCB
imeandaa matamasha mawili ya kukata na shoka ambayo yatafanyika katika
msimu huu wa sikukuu katika Mikoa ya Dar es Salaam na Iringa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyomella, alisema matamasha hayo makubwa ya muziki wa kizazi kipya yatafanyika katika mikoa ya Dar e salaam na Iringa chini ya wasanii Diamond Platinumz, Rayvanny, Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.
“Kama
mnavyoelewa msimu huu huwa umeambatana na shamrashamra mbalimbali za
sikukuu na mitoko ukiwa na familia yako, Desemba 24 kutashushwa shoo ya
nguvu katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Hotel ambapo kutakua na
tamasha la kihistoria la “Vodacom Wasafi Beach Party” na Iringa tamasha
litafanyika siku ya Krismasi katika uwanja wa Samora na matamasha yote
yataanza saa nane mchana”. Alisema.
Mwiyombella alisema burudani hii ya muziki inakwenda sambamba na promosheni ya “Nogesha Upendo” http://vda.cm/nogeshaupendo
ya Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom
zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo
fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha haya
makubwa katika msimu huu wa sikukuu.
“Ili
kujishindia tiketi ya bure anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni
kupiga*149*01# kisha nunua kifurushi chochote cha Vodacom na moja kwa
moja atakua ameingia katika droo ya kuweza kujishindia tiketi. Zawadi
nyingine kemkem kupitia promosheni ya Nogesha Upendo ni fedha taslimu,
muda wa maongezi, Vifurushi vya intaneti (Mb)”.Alisema.
Naye
Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika anga za kimataifa,
Diamond Platinumz akiongea kwa niaba ya wasanii wa WCB alitoa wito kwa
wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya
shoo hizo kwani zitakuwa ni shoo za kihistoria katika mikoa hii miwili
kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB,Napenda kuwahakikishia
mashabiki wetu kwamba tutakamua vilivyo tukiwa na wasanii wenzangu wote
wa WBC kwa “Kunogesha Upendo” Alisisitiza Diamond.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment