Unakumbuka
lile sakata la mmoja wa wagombea kiti cha Urais nchini Marekani
kukumbwa na kashfa ya kutumia anwani ya barua pepe binafsi kufanya
shughuli za Serikali?
Au
umeshawahi kuona barua pepe (Pengine unayo unaitumia) ikiwa na
mchanganyiko wa herufi na namba, mfano, wateja wako watajali kweli ukiwa
na barua pepe brian255@yahoo.co.tz au brian.mbunde@kampuniyako.co.tz?
Sasa
Extreme Web Technologies ni mshirika rasmi wa Microsoft kwa upande wa
Tanzania na wanakufahamisha kwamba katika hii ulimwengu tunaoenda nao wa
digitali unapokuwa na professional business email unajenga uaminifu
katika biashara yako na unaonekana uko smart sana.
Pengine bado unajiuliza “Professional Email” ni nini, ukiangalia mfano hapo juu wa barua pepe ya brian.mbunde@kampuniyako.co.tz inaonesha jina kamili la mhusika na kuna domain ya kampuni.
Hii
inamaanisha kwamba hauwafanyi watu waone jina lingine tofauti na jina
lako halisi hivyo kuwapa mitazamo tofauti linapokuja suala la biashara
(Uaminifu) na hapo ndipo Microsoft O365 inakuletea kile unachohitaji
mahali unapokuwa.
Unapataje Barua pepe ya Biashara?
Jinsi
ya kupata ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kuwa tu na email na
kisha kuwa na “domain” ambayo imehifadhiwa mahali (server). Baada ya
hapo utapewa uhifadhi kumbukumbu unaofikia 1 TB, kuwekewa Microsoft
Office kwenye kompyuta mpakato yako na kwenye simu yako pia. Huduma
nyingine zinahusisha “HD Video Conferencing”.
Kama
bado huna uhakika na umuhimu wa “Professional Email” hizi hapa sababu
tano za msingi za kwanini unatakiwa kuwa na barua pepe maalum kwa ajili
ya biashara yako.
1.
Kuonesha Uweledi; “Professional Email” inaonesha kwamba biashara yako
imeimarika na inaendeshwa kwa uweledi wa hali ya juu, lakini pia
inaonesha uko makini na biashara yako na itakuwepo siku zote. Ukiwa na
barua pepe ya kawaida unawapa mashaka wateja kama kweli biashara ni
halali na una uzoefu.
2.
Kujenga Picha Kubwa; Barua pepe ya kawaida inaweza kuonesha kwamba
biashara yako ni mpya au ndogo. Ukiwa na barua pepe maalum inaleta picha
ya kwamba biashara yako ni kubwa na kuipa muonekano wa kampuni haswa.
Pia kutengeneza barua pepe kwa ajili ya makundi mbalimbali katika
biashara yako mfano finance@kampuniyako.co.tz, info@kampuniyako.co.tz, strategy@kampuniyako.co.tz itaimarisha biashara yako.
3.
Kujenga uaminifu na Imani; Miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la
wizi wa mtandaoni, hivyo wateja wengi huru kutuma taarifa binafsi kwenye
barua pepe kama brian@yahoo.com,
lakini unapokuwa na barua pepe maalum kwa ajili ya biashara yako unampa
mteja hali ya kujisikia salama na uhakika kwa wateja kuwa biashara yako
ni halali.
4.
Haina Gharama...Ni Rahisi; Unaweza kuwa na barua pepe maalum kwa
jitihada ndogo tu kupitia mtoa huduma za domain au tovuti bure au kwa
gharama ndogo sana. Faida kubwa ya kuwa na kusajili domain yako ni
kwamba itakuwa pamoja na biashara yako.
5.
Kukuza Biashara Yako; Faida nyingine ya kutumia barua pepe maalum ni
kwamba kila wakati unapowasiliana na mtu/mteja unakuza biashara yako.
Hivyo kama ulikuwa unafikiria barua pepe maalum ni kwa makampuni makubwa
tu, usifikirie hivyo tena.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment