SIKU moja baada ya gari la Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini
kupitia Chadema kumgonga Recho Lutumo (14) na kumuua, mbunge huyo
ameomba radhi familia ya marehemu, anaandika Mwandishi Wetu.
Ajali hiyo ilitokea katika Barabara Kuu ya Zambia kwenye eneo la Iyunga
ambapo Neema alikuwa akivuka kwenye kivuko cha waenda kwa miguu.
Gari la Sugu lilikuwa likiendeshwa na Gabriel Andrew (43) akitokea jijini humo kwenda katika Uwanja wa Ndege wa Songwe (SIA).
Wakati wa maandalizi ya maziko ya Neemba akiwa pamoja na ndugu wa
marehemu, mbunge huyo alieleza masikitiko yake ya kumpoteza binti kwenye
ajali hiyo.
Sugu amesema moja ya matukio mabaya kutokea akiwa mbunge ni la kupoteza Neema ambaye ni mkazi wa Mbeya na raia wa Mtanzania.
“Naomba mnisamehe. Kifo hiki kimeniumiza, nawaomba radhi ndugu
wanafamilia na wananchi wa Mbeya,” ameeleza Sugu kwenye msiba huo.
Dhahiri Kidavashari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amesema Gabriel ambaye ni dereva wa Sugu, anashikiliwa na jeshi hilo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
Post a Comment