KIJANA
mwenye umri wa 23 na mpenzi wake, bibi mwenye umri wa miaka 60 , wakazi
wa kijiji cha Tentula, Kata ya Ikozi wilayani Sumbawanga, wanashikiliwa
na polisi wakihutumiwa kumshambulia na kumuua kikatili jirani yao
aitwae Desder Justino (23) kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa
mapenzi.
Inaelezwa kuwa, Justino pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bibi huyo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo na
kueleza kuwa mauaji hayo yalitokea Desemba 21 mwaka huu saa nne asubuhi
katika nyumba ya mwanamke huyo iliyopo kijijini Tentula.
Taarifa
kutoka kijijini humo zinadai kuwa, mwanamke huyo licha ya umri wake
kuwa mkubwa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana hao wawili wa
rika moja.
Kamanda Kyando hakuwa tayari kutaja majina ya wapenzi hao ambao ni watuhumiwa wa mauaji kwa sababu za uchunguzi.
Lakini
alisema mwanaume ana umri wa miaka 23 huku mpenzi wake ana umri wa
miaka 60. Akielezea zaidi, Kamanda Kyando alisema siku ya tukio Justino
alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano
naye wa kimapenzi na kumkuta kijana mwingine (mtuhumiwa), na hapo ndipo
ugomvi ukaibuka baina ya vijana hao.Alisema Justino alijeruwa kichwani.
“Wawili
hao yaani wapenzi hao (mwanamke na mwanaume) walimshambulia Justino
(Desder) kwa kumpiga kichwani na kitu chenye ncha kali na kumjeruhi
vibaya na alikufa akiwa anatibiwa hospitalini,” alisema Kamanda
Kyando na kuongeza kuwa, watuhumiwa hao wanashikiliwa na watafikishwa
mahakamani uchunguzi wa awali utakapokamilika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment