Najua watanzania na waafrika wote walikuwa wanahamu ya kufahamu mshindi
wa Miss World 2016 atakuwa ni mrembo kutoka nchi gani, mashindano hayo
ambayo yamefanyika Washington Marekani, Afrika ilipata nafasi ya nchi za
Kenya na Ghana kuingia TOP 20.
Muda ulifika na waandaaji wa Miss World walitangaza mshindi ambapo Miss
Puerto Rico ndio alifanikiwa kushinda taji la Miss World 2016, lakini
muwakilishi wa Tanzania Diana Edward kwa bahati mbaya hakufanikiwa
kufika nafasi za juu.
Hata hivyo Afrika Mashariki imepokea good news baada ya nchi ya Kenya
kufanikiwa kuingia TOP 5 na ndio nchi pekee ya Afrika iliyofanikiwa
kuingia TOP 5, huku Miss Dominician Republic akishika nafasi ya pili na
Miss Indonesia akishika nafasi ya tatu.
TAZAMA VIDEO ILIVYOKUWA:
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment