Mchungaji
maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian
lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo
cha kuwanywesha Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu.
Kwa
mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye
ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na
wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku
akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.
“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,” – Mchungaji.
Pia alisema
kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na
wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa
Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa
Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa
“Mtu
akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa
ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na
kufariki.
“Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”
“Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”
Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata..
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment