WANAWAKE
wengi watakiri kuwa mavuzi ni kero hasa katika kudumisha usafi au
kuonekana nadhifu wakati wa mahaba. Sababu hii imewapelekea wengi
kutafuta mbinu na bidhaa mbalimbali kuondoa nywele hizi na kuhakikisha
kuwa sehemu hii inaoenekana wazi na nyepesi vilivyo kwa kunyoa kwa
mashine, krimu au hata nyembe huku mabinti wengine wakiamua kuvumilia
uchungu unaoambatana na utaratibu wa kutumia mchanganyiko maalum wa nta
(waxing), mtindo maarufu siku hizi hasa kutokana na sifa yake ya kuacha
sehemu iliyonyolewa ikiwa nyororo na laini kwa muda mrefu. Aidha kampuni
zinazotengeneza bidhaa hizi zimekuwa na kibarua cha kutoa bidhaa mpya
kila kuchao, nia ikiwa kuvutia soko la wanawake wanaotaka sehemu hiyo
kusalia nyororo kama ya mtoto mchanga. Lakini huku majarida ya wanawake
yakiendelea kuchapisha makala yanayopiga vita nywele hizi, maelfu ya
wanawake katika sehemu zingine ulimwenguni wanatafuta mbinu za kuhifadhi
vichaka hivi. Korea Kusini ni mojawapo ya nchi ambapo idadi ya wanawake
wanaofanyiwa upasuaji kuongeza au kubandikwa nywele hizi inazidi
kuongezeka kila kuchao. Kulingana na makala yaliyochapishwa mwezi
uliopita na Refinery29, mojawapo ya majarida ya masuala ya kimitindo na
mahusiano nchini humo, asilimia 10 ya wanawake katika taifa hilo
wanakabiliana na upungufu wa mavuzi hasa ya kinenani, hali inayofahamika
kama “pubic atrichosis,” suala ambalo limewakosesha wengi usingizi.
Mvuto Hii ni hasa ikizingatiwa kuwa utamaduni nchini humo unahusisha
nywele hizi na uwezo mkubwa wa kuzaa na kudumisha mvuto wakati wa
mahaba. Pia inasemekana kuwa wanaume wengi nchini humo wanaamini kuwa ni
bahati mbaya kushiriki ngono na mwanamke asiye na mavuzi, suala ambalo
limepelekea mabinti wengi kukimbilia utaratibu huu ili kujiongezea sifa
za kike. Inasemekana kuwa asilimia 74 ya wanawake nchini humo
wamefanyiwa utaratibu huu, huku idadi ya wanawake wanaofanyiwa upasuaji
kuongezewa au kubandikwa mavuzi ikiongezeka kwa asilimia 160. Hii ni
licha ya utaratibu huo kugharimu dola 2,000 sawa na Sh180, 000. Ni
mtazamo ambao hata hivyo unaotofautiana vikali na utafiti uliofanywa
miaka mitatu iliyopita nchini Amerika kubaini hisia za wanawake kuhusu
nywele hizi. Udadisi huo uliofanywa na Dkt Debby Herbenick, mtafiti wa
kisayansi katika Chuo Kikuu cha Indiana na mwalimu wa afya ya kijinsia
katika taasisi ya Kinsey nchini Amerika, ulionyesha kuwa wanawake wengi
nchini humo wanaamini kuwa kuondolewa kwa nywele hizi kunaimarisha
ashiki. Hata hivyo suala la kuwepo au kutokuwepo kwa mavuzi halijazua
mdahalo nchini Korea Kusini au Amerika pekee bali hata hapa nchini
ambapo watu wana hisia tofauti kuhusu mavuzi. Kuamsha ashiki Kulingana
na Charles, mwanamke aliyeotesha nywele hizi huamsha nyege zaidi
akilinganishwa na yule aliyezinyoa kabisa. “Wakati wa mahaba, nywele
hizi zitakupa hisia kuwa mwenzako ni mwanamke kamili, tofauti na binti
aliyenyooka kabisa katika sehemu hii,” asema. Lakini kulingana na
Vincent, mhudumu katika duka moja la jumla jijini Nairobi, hakuna raha
inayotokana na mgusano wa nywele hizo wakati wa mahaba. Anasema kuwa
mkwaruzo huo huhusishwa na jinsia ya kiume kumaanisha kuwa mwanamke
anapaswa kuwa laini vilivyo. Kulingana naye nywele hizo ni ishara ya
uchafu na kuwa mwanamke huyo hajishughulikii vizuri. Japo hakubaliani na
sehemu hiyo kufanana na kichaka, James, mchuuzi wa bidhaa za rejareja
jijini anasema kuwa binti anaponyoa hapaswi kuziondoa zote. “Badala ya
kunyoa kabisa, zipunguze kuhakikisha kuwa sehemu hiyo haikwaruzi wakati
wa mahaba na wakati huo huo zile hisia za mapenzi zinadumishwa,”
aeleza.Jecinter, mhudumu wa saluni moja viungani mwa jiji la Nairobi,
asema kuwa nywele hizo ni kero kwani husababisha changamoto inapowadia
wakati wa kudumisha usafi. “Ni sababu ambayo huenda imepelekea idadi ya
wanawake wanaotembelea saluni yetu kufanyiwa 'waxing’ kuongezeka,”
aeleza. Lakini katika makala yake 'End to War on Pubic Hair’, Dkt Emily
Gibson wa Chuo Kikuu cha Western Washington, nchini Amerika anatoa wito
kusitisha vita dhidi ya nywele hizi. Kulingana na mtaalamu huyu, kasumba
ya kulainisha eneo hili imesababishwa na nadharia zinazohusisha urembo
na mavazi ya kuogelea kama vile 'bikini’, mitindo inayomhitaji mwanamke
kuwa nyororo katika sehemu hii kumaanisha kuwa nywele hizi hazifai.
Anasema kuwa tafiti kadha za kimatibabu zinaashiria kuwa nywele hizo
kamwe haziathiri usafi wala afya ya sehemu hii, na badala yake husaidia
dhidi ya mikwaruzo inayosababisha majeraha. Athari Anasema kuwa kinena
kilichonyolewa hukumbwa na hatari kubwa ya kupata maambukizi ya maradhi
kama vile 'herpes’, kutokana na majeraha ambayo huwa wazi kwa virusi
vinavyopatikana kwenye viungo vya uzazi. Kulingana na Chris Hart,
mshauri wa masuala ya mahusiano, suala la mahaba limewakanganya wengi
kudhani kuwa nywele hizi huimarisha maisha haya. “Mahaba ni suala la
kisaikolojia. Kuna watu wanaofurahia nywele hizi ilhali kuna wengine
ambao hisia zao za mahaba huamshwa na mazingira mepesi, kumaanisha kuwa
hakuna kiwango kamili cha jinsi sehemu hii inavyopaswa kuwa,” aeleza
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment