Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake.
Siku moja baada ya DW kuitaja ngoma aliyoshirikishwa na marehemu Papa Wemba, Chacun Pour Soi kuwa imefunga mwaka kwa kuwa namba moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kidogo aliyowashirikisha P-Square nayo imefunga mwaka kwa kishindo.
Wimbo
huo umekuwa wimbo wa mwaka katika kituo cha redio cha Radio Afro cha
Australia, baada ya kuzishinda nyimbo za magwiji wengi wa Afrika
wakiwemo Wizkid, Davido, Tiwa Savage na wengine kibao.
Diamond
ameshukuru kwa nafasi hiyo kwa kusema, “Thank you AUSTRALIA thank you
RADIO AFRO…. KIDOGO ft P -SQUARE Song of the Year #RADIOAFRO.”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment