JESHI la Polisi Zanzibar linatarajia kumfikisha mahakamani mtu anayedaiwa kumkashifu Mtume Muhammad (S.A.W).
Mtuhumiwa
huyo, Dk. Abdallah Saleh Abdallah (50), mkazi wa Kikwajuni mjini
Unguja, baada ya kutoa maneno hayo ya kashfa juzi na kusambaa kwenye
mitandao ya kijamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Kamishna wa Jeshi la Polisi
visiwani hapa, Hamdan Omar Makame, alisema walimtia mbaroni daktari huyo
wa binadamu baada ya taarifa zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii,
ikiwamo wa Facebook.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkashifu Mtume Muhamad na waumini wa dini ya Kiislamu.
“Tumemkamata
mtuhumiwa na tayari tumeshakamilisha kila kitu, ikiwamo taarifa za
upelelelezi. Hivyo kilichobaki ni kumfikisha makahamani tu ili aweze
kujibu mashtaka yake,” alisema Kamishna Makame.
Akiongezea
kuhusu ukusanyaji wa taarifa za upelelezi, alisema wamelazimika
kumshikilia kijana Ali Juma Makame (30) mkazi wa Michenzani mjini hapa
ambaye anatuhumiwa kusambaza video hizo mitandaoni.
“Tunawanasihi
waumini wa dini ya Kiislamu kutokubali kuyumbishwa na kufanya
maandamano kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria, ni bora
kujiepusha na jambo hili kwani tayari vyombo vya ulinzi vimeshachukua
hatua kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Post a Comment