Loading...

WABUNGE Wavurugana Tena Bungeni Nchini Kenya


NAIROBI, KENYA: Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira mapema leo asubuhi desemba 22, 2016 katika Mji Mkuu wa Nairobi nchini humo kwa madai kuwa baadhi yao wamekuwa wakinyanyaswa

Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyingine katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwakani.

Serikali inataka mfumo ambao utasaidia shughuli ya kuhesabu kura iwapo mfumo wa kielektroniki utafeli lakini upinzani unasema kuwa ni njia moja wapo ya kuiba kura.

Awali hatua ya kuupigia kura mswada huo ili ufanyiwe marekebisho ilisababisha kuzuka kwa ghasia juzi, Jumanne.

Upinzani wa CORD umesema kuwa mmoja ya wabunge wake aliumizwa hadi kuvuja damu usoni kufuatia vurugu na wabunge wa chama tawala mapema siku ya Jumatano.

Cord imeenda mahakamani ikitaka marekabisho hayo kutopitishwa bungeni lakini chama tawala kimepitisha marekebisho hayo.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright KISWAGA BLOG
Back To Top